Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Gazeti la Kifaransa la Ouest-France limeandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, waziri mkuu wa Australia Scott Morrison ametangaza kuwa, "nina stahamala kubwa, na ninao uwezo wa kulihimili hili."
Hata hivyo Scott amoeongeza kuwa hawezi kukubali "tuhuma" zinazolenga utaifa wote wa Australia.
Siku ya Jumapili ya tarehe 31 Oktoba Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alimtuhumu Morrison kwamba amesema uongo kuhusu mazungumzo ya siri kuhusu makubaliano ya kiulinzi ya AUKUS yaliyofikiwa baina ya Australia, Marekani na Uingereza.
Scott Morrison ameongezea kwa kusema :"Sisi tulichukua uamuzi kulingana na maslahi ya Australia, kwamba tusiendeleze mkataba na shirika la Ufaransa la Naval Group, baada ya mwezi Desemba uliopita."
Waziri Mkuu wa Australia amesisitiza kuwa anachukua maamuzi magumu ili kuweza kuwa na hakika kwamba Australia inakuwa na uwezo bora kabisa wa kiulinzi.../
342/